Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
LICHA ya mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa,  kuwapigia simu viongozi wake juzi Jumanne, lakini wameahidi kuendelea kumchunguza kwa kuhusishwa na kutimkia nchini Afrika Kusini kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, tofauti na alivyoomba ruhusa ya kushugulikia matatizo ya familia yake.

Wiki iliyopita Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha alikaririwa na Mwanaspoti kuwa alisikia Ngassa ametimkia Afrika Kusini na alipojaribu kumtafuta kwenye simu yake hakupatikana.

“Nimepigiwa simu na Ngassa usiku wa juzi Jumanne , tumezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kumuuliza maendeleo  ya matatizo ya familia yake, lakini hilo  halinifanyi   niache kuendelea kuchunguza ukweli juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake,” alisema.

Tiboroha alisema endapo kama itabainika  mchezaji wao kafanya kosa hilo atawajibishwa ili iwe mfano kwa wachezaji wengine kuzingatia nidhamu ya kazi zao za kufuata utaratibu unaotakiwa na siyo kufanya mambo kiholela.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top