Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.
 
Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa  na pia haina tija katika tasnia ya filamu.
 
Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofanyika  kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top