Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
1292434-27841551-1600-900
Klabu ya Arsenal imemruhusu mshambuliaji wake Lukas Podolski kujiunga na mabingwa wa zamani wa ulaya Inter Milan zikiwa zimepita siku chache tangu kocha wa Arsenal Arsene Wenger akanushe taarifa za mshambuliaji huyo kuondoka.
Podolski anajiunga na Inter baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal ambapo mara nyingi amejikuta akiwa mshambuliaji wa akiba ambaye mara zote amekuwa akitokea benchi pamoja na kuwa na rekodi nzuri ya kufunga kulingana na nafasi ndogo anayopewa.
Lukas Podolski ameondoka Arsenal na kujiunga na Inter Milan baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Lukas Podolski ameondoka Arsenal na kujiunga na Inter Milan baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Mshambuliaji huyo Mjerumani ataichezea Inter kwa mkopo wa miezi sita na baada ya hapo atakaa chini na uongozi wa klabu hiyo na kuchagua kama angependa kujiunga nao moja kwa moja.
Siku chache zilizopita kocha wa Arsenal Arsene Wenger alikanusha taarifa za kuondoka kwa Podolski baada ya kuulizwa na waandishi wa habari ambapo jibu la kocha huyo mfaransa lilikuwa ‘hapana Podolski hataondoka’.
Lukas Podolski akiwa na mashabiki wa Inter Milan kwenye uwanja wa ndege wa Milan baada ya kuingia akitokea London juzi.
Lukas Podolski akiwa na mashabiki wa Inter Milan kwenye uwanja wa ndege wa Milan baada ya kuingia akitokea London juzi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top