Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
gb9jo2dq5dkaawtmbgxk
Tumezoea kukutana na zile story za mitaa mbalimbali D’salaam, watu kuuziwa sabuni ambazo hubadilishwa na matapeli ambao wanajifanya wanauza simu mtaani.

Wengi tukienda madukani kununua vitu mara nyingi tunakuwa na imani na vitu ambavyo tunavinunua vikiwa vimefungwa ndani ya boksi, lakini kumbe kuna haja ya kufungua kabla ya kuondoka dukani ili yasikukute yaliyomkuta jamaa mmoja maeneo ya Colorado, Marekani.
PS4-Rocks
Igor Baksh  alinunua Playstation 4 zawadi kwa mtoto wake, kufika nyumbani alifungua na kukutana na mawe yaliyofungwa vizuri ambapo ukiangalia kwa haraka unaweza kuona ni kama dawa za kulevya.
Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda maduka yalikuwa yamefungwa aliamua kwenda duka la kampuni hiyo lililopo jirani kwa ajili ya kurudisha mawe hayo, wakamwambia arudishe kwenye duka husika walikomuuzia, siku ya pili alipoenda dukani walikataa kumbadilishia na kusema kuwa hawana ushahidi kwamba kile walichomuuzia jana yake kilikuwa mawe.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top