Mwanamke aitwaye Maria Haule mkazi wa Kijiji cha Muhukuru Songea vijijini mkoani Ruvuma ameuawa kwa kukatwa na shoka kichwani na mume wake aitwaye Salvatory Ndimbo na kisha mwili wake kuutupa mto Mkurumo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela anasema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kimapenzi ambapo marehemu Maria Haule mwenye miaka arobaini alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine aitwaye Anzekula na kutaka kuachana na mumewe Salvatory Ndimbo mwenye miaka sitini.
Jeshi la polisi linaendelea kumsaka mume wa marehemu Maria Bw. Ndimbo mbaye ametoroka baada ya kufanya unyama huo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment