Wakali hao walionesha kumpigia saluti Diamond baada ya kukutana naye kwenye tamasha la utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Afrika lililofanyika Lagos, Nigeria, usiku wa kuamkia Januari 9, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache kabla ya shoo kuanza, P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko aliyofikia jijini humo na kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri baadhi ya vitu vya kimaendeleo.
Chanzo hicho kilisema, P-Square walionekana kuvutiwa zaidi na juhudi binafsi za Diamond kiasi cha kuweza kuipeperusha bendera ya Afrika Mashariki katika levo za kimataifa.
“Jamaa walipomuona tu hotelini waliguswa sana na juhudi zake binafsi maana wanatambua jinsi gani muziki ulivyokuwa mgumu kuuvusha nje ya nchi yako lakini kwa kuwa Diamond ameweza, walimpigia saluti,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data za ndani kwa kusema, mbali na kumpigia saluti, P-Square walionesha wako tayari kumsapoti Diamond kwa kumpa nafasi ya kufanya nao kazi yaani kolabo.
“Wamempa nafasi ya kufanya naye kazi pale atakapojisikia kutokana na mipango yake, kama akiamua kufanya sasa au baadaye ni uamuzi wake lakini jamaa (P-Square) hawana kinyongo naye lengo lao ni kuona muziki wa Afrika unateka dunia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

Mbali na P-Square, mastaa mbalimbali wa Nigeria walimuibukia Diamond hotelini hapo akiwemo Mr Flavour na Jude Abaga ‘M.I’, ambao walimpa pongezi Diamond kwa kujua kumiliki vyema jukwaa kwani wamekuwa wakifuatilia shoo zake hasa anapotupia video zake mitandaoni.
Ulipofika wakati wa kupanda jukwaani, Diamond aliitikisa Nigeria kwani alionesha vitu vya tofauti wakati akiimba nyimbo zake na kuwafanya Wanigeria na waalikwa mbalimbali wapigwe na butwaa huku wengi wakiishia kumpigia makofi na shangwe la kufa mtu.
Mwanahabari wetu alimcheki Diamond kupitia mtandao wa WhatsApp ambapo aliwashukuru mastaa hao wa Nigeria kwa upendo wao na kuahidi kuendelea kufanya maajabu zaidi katika levo za kimataifa.
“Wana wamenisapraizi hotelini, tumepiga stori nyingi, wameonesha wanakubali kile ambacho mimi nafanya, jukwaani nimefanya vizuri, watu na heshima zao mwishoni walipiga makofi kuonesha wamekubali.
“Kuhusu kolabo na P-Square, ni mapema sana kuzungumzia kwa kuwa nina mipango mingi ya kufanya mwaka huu, mashabiki wakae mkao wa kula, nikiona inafaa, nitafanya nao maana wao hawana shida na mimi,” alisema Diamond.
Awali, kabla Diamond hajakutana na P-Square, alishirikiana na mkali mwingine wa Nigeria, Davido katika wimbo wake wa Number One Remix ambaye inaaminika kwa umaarufu na uwezo wa kimuziki yupo chini ya P-Square.
Post a Comment
Post a Comment