Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwigizaji wa filamu hapa bongo, Aunt Ezekiel  amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na mwigizaji huyo, amethibitisha kwamba  ni kweli ujauzito wa Aunty sio wa mume wake ni wa dansa wa Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moses Iyobo.
“Ni kweli ujauzito wa Aunty ni wa mpenzi wake na si mumewe. Unajua anatoka na Iyobo na wawili hao bado wanaonekana pamoja, hafanyi tena safari za Dubai ambako ndiko mumewe aliko,” kilisema chanzo hicho.
Aidha Aunty Ezekiel alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.
“Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu,” alidai Aunt.  
Ngoja tusubiri kama bado kuna ndoa hapa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top