
Binti mmoja mwenye umri wa miaka 19, Rukia Ally anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kaka yake wa kuzaliwa, Said Ally wote wakazi wa Tegeta Mivumoni jijini Dar es Salaam, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kijana huyo kutaka kudhibiti tabia zisizofaa za dada yake huyo, tukio lililotokea usiku wa Januari 24 mwaka huu. Inadaiwa kuwa siku hiyo, msichana huyo hakuwa amerudi nyumbani kwa siku tatu, hivyo aliporejea saa tatu usiku, kaka yake alimuuliza alikokuwa lakini alishindwa kutoa majibu ya kueleweka, kaka huyo alimchapa na fimbo mguuni kama ishara ya kumkanya, lakini inadaiwa Rukia alichomoa kisu alichokuwa amekificha nguoni mwake na kumchoma nacho upande wa kushoto wa kifua chake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment