March 29, 2025 07:16:40 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Muonekano wa basi la Dar Express likiteketea kwa moto leo mchana eneo la Kwamakocho, Kijiji cha Kimange, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Linahesabika kama tukio jingine la Basi kuwaka moto katika rekodi za mabasi yaliyowaka moto yakiwa safarini nchini Tanzania wakati yakiwa na abiria.

Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Pwani SACP Jafari Ibrahimu ni kwamba basi hilo la kampuni ya Dar Express liliwaka moto likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa limejaa abiria.

DX 4

Amesema >>> ‘Ni kweli basi la Dar Express saa saba mchana kwenye kijiji cha Kimange ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Pwani lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote, hawakuwahi kulizima, hakuna yeyote aliejeruhiwa‘


Kamanda Ibrahimu amesema kuwa abiria wote waliokuwemo ndani ya basi hilo wako salama.

Eneo la Kwamakocho lipo katikati ya eneo la Mandela na Mbwewe mkoani Tanga.

RPC Jafari Ibrahimu amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na akasema uchunguzi unaendelea.

TAZAMA VIDEO HAPA UONE JINSI BASI LILIVYOKUWA LINATEKETEA KWA MOTO

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
09 May 2015

Post a Comment

 
Top