March 19, 2025 10:41:41 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Matukio  ya  mauaji  ya  kikatili  dhidi  ya  wanawake   katika  wilaya  ya  Butiama  yameanza kurejea upya  baada    ya  mwanamke   mmoja   mkazi   wa   kijiji   cha   Maneke  katika   halmashauri   ya  Musoma mkoani  Mara    kuuawa  kinyama   kwa   kukatwa   mapanga   tukio  ambalo  limehusishwa   na  imani za  kishirikina.

Kamanda  wa  polisi  mkoa wa  Mara  kamishna  msaidizi  wa  jeshi  la  polisi  ACP  Philip Alex kalangi, amesema kuwa  mwanamke   huyo  Mwadawa   Elias    mkazi    wa   kijiji   hicho   cha   Maneke, ameuawa   baada    ya kuvamiwa    akiwa   amelala  nyumbani   kwake    majira   ya   usiku   na   watu   zaidi    ya   wanne   kisha  kuanza   kumshambulia  kwa   kumkata kata  kwa  mapanga.

Mwanzoni  mwa  mwaka   jana   zaidi   ya  wanawake   40   katika  tarafa   ya   Nyanja  wilaya   ya  Butiama   waliuawa  kinyama  kwa   kuchinjwa  na  wengine  kukatwa  mapanga  kisha    wauaji    kuchukua   baadhi    ya viungo    vya  miili   ya  marehemu  kwa imani    hizo   za   ushirikina   na   kusababisha    hofu    kubwa    kwa  jamii    katika  eneo  hilo   kabla   ya   hatua  mbalimbali    kuchukuliwa   na   serikali   kupitia   vyombo   vyake  vya   dola   katika  kudhibiti  ukatili  huo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
23 Jan 2015

Post a Comment

 
Top