Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Zaidi ya watu 40 wamenusurika kifo huku mmoja akikatika viungo vya  miguu na wengine kujeruhika vibaya baada ya lori  moja lilionekana kuwa ni la jeshi kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya COSTA la Ubungo -Tegeta eneo la Tegeta jijini Dar es salaam.
Tukio hilo limevuta hisia za mamia ya wakazi wa Tegeta huku baadhi ya mafundi gereji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu kukata mabati ya magari kwa nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani ya COASTA hiyo kusuru abiria walioonekana kunasa katika vyuma vya magari hayo.
 Baadhi ya mashuhuda na dereva wa COSTA pamoja na kuomba eneo la kibaoni kuweka njia ya mzunguko maarufu kama ROUND ABOUT kwa lengo la kuepusha madereva wanao lazimika kugeuza kwa dharura katika njia kuu maarufu kama UTAN kutokana na njia hiyo kukosa fursa ya kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo.
 Pia wamemtupia lawama Dereva wa Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla ya kufanya hivyo.
Kamanda wa polisi mkoa kipolisi Kinondoni  Kamilius Wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kutoa taarifa mara baada ya uchunguzi kufanyika.
Chanzo:-ITV

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top