Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

WAKAZI wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamekumbwa na wasi wasi mkubwa, kufuatia taarifa ya mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na kutapika na kuibua hofu kuwa huenda ugonjwa huo ni kipindupindu.
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kuwa katika kipindi cha Januari mosi mpaka sasa watu watatu wameripotiwa kufa kutokana na ugonjwa huo ambapo wagonjwa 20, wamekutwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni huku 17 kati yao wakitoka Kata ya Kibirizi.
Kufuatia taarifa hizo mtandao huu umezungumza na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Dr.Makris Yakayashi, ambaye alisema kuwa bado haijathibitika kama ugonjwa huo ni kipindupindu ingawa amekiri kuwepo kwa wagonjwa wenye dalili za ugonjwa huo.
Alisema kuwa tangu siku ya Ijumaa ya Januari 2 hadi 6 mwaka huu kulikuwa na wagonjwa 12 wenye dalili za kipindupindu waliolazwa katika hospitali ya Maweni huku wengi wao wakitoka Manispaa ya Kigoma Ujiji na baadhi wakitoka katika vijiji vya Mtanga na Mwakizega, ingawa ameeleza kutokuwa na taarifa za vifo.
Chanzo:-kigomalive

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top