Na Musa Mateja
BAADA ya kudaiwa kuwa wapenzi na kisha habari hizo kufifia, hatimaye penzi la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, limeibuka upya ambapo safari hii Nay ameamua kufunguka hadharani.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao walianzisha uhusiano wao mwishoni mwa mwaka jana na sasa mapenzi ndiyo yamekolea hadi kufikia hatua ya Nay wa Mitego kuanika hisia zake mtandaoni.
“Wamekuwa wakibanjuka kwa siri sana si unajua Nay ana mchumba wake Siwema, bado hajafanya maamuzi magumu ya kumtosa,” kilisema chanzo chetu.
Paparazi wetu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Nay wa Mitego kwenye mtandao wa Instagram ambao ulionyesha wakiitana kwa majina ya wapendanao kuonesha dhahiri wawili hao ni wapenzi.
Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo muda mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia kisha Nay akaifuta posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.
Alipoulizwa Wolper kama kwa sasa ameamua kutulia na Nay wa Mitego na mipango ya uhusiano wao ipoje, alikataa kufunguka moja kwa moja.“Kiukweli Nay ni mshikaji wangu tu, unajua nini? Kwa sasa siko tayari tena kumwanika bwana au mchumba wangu kama nilivyofanya mwanzo kwa Dallas, nitakuja kumweka wazi labda mwanaume nitakayezaa naye au atakayenioa kabisa,” alisema Wolper.
Kwa upande wake Nay alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wolper na hatua ya kuunadi uhusiano wao mtandaoni huku ikifahamika kuwa ana mchumba mwingine, hakutaka kufafanua zaidi ya kujibu:
“Mimi huwa siangalii nani atasema nini wala atafikiria nini, mimi nilimmisi Wolper wangu, sikuwa na namna zaidi ya kutumia peji yangu kama nilivyofanya, tena siku hiyo alikuwa hapatikani hewani nikaamua kumtupia mtandaoni bila hofu kwani ni mtu wangu wa karibu na siogopi kitu juu yake,” alisema Nay wa Mitego.
~Gpl
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Mapenzi Yamtokea PUANI Davina24 Jul 20150
Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya amedaiwa kutoswa na mwanaume aliyemuachanisha na mumewe...Read more ?
- Kigogo Mpya Wa Jack Wolper Anaswa02 May 20150
Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibong...Read more ?
- Vanessa Mdee: Japo Nina Boyfriend (Jux) ila Sasa Hivi Siwezi Kuwa na Mtoto…Ifahamu Sababu26 Apr 20150
Muimbaji wa ‘Nobody But Me’ Vanessa Mdee a.k.a Vee Money ambaye hivi sasa ameweka wazi uhusiano w...Read more ?
- Naima wa Aslay Ndani ya Penzi Zito na Kipa wa Simba Manyika JR ..Adaiwa Kumshusha Kiwango cha Mpira Awapo Uwanjani21 Apr 20150
Baada ya kuwapa majibu wale wote ambao waliokua wanadai kwamba ameshuka kiwango, hivi sasa watu ...Read more ?
- Mahaba Niue! Siri ya Mapenzi Yao Iko Moyoni Mwao Wenyewe17 Apr 20150
Mastaa wengi wamekuwa wakiingia kwenye uhusiano na kufanya siri kubwa. Wapo ambao wanaonekana dhah...Read more ?
- Hatimaye Shamsa Ford Atoboa Kuwa Nay ndio “EndlessLove” Wake14 Apr 20150
Staa mrembo wa Bongo Movies Shamsa Ford ambae siku za hivi karibuni alikanusha waziwazi alipoku...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment