Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Aunty Ezekiel 
Mwigizaji wa filamu Aunt Ezekiel ambae kwasasa ni mjamzito, amechukizwa na kitendo cha baadhi ya watu ambao ni followers wake kwenye mtandao wa Instagram kumshambulia na kuzua malumbano ya maswala ya Dini, hii ilitokea hapo jana (Jumapili) mara baada ya mwigizaji  huyo kubandika picha (hiyo hapo juu) mtandaoni na kuandika maneno haya “When Jesus say YES no body can say No …..Happy me”

Kitendo hiki kiliwafanya baadhi ya watu wenye imani tofauti na ukristu kuibuka na kuanza kumshambulia kwa maneno ambayo yalikuwa ya kiponda imani yake na huku baadhi ya watu nao wakijibu mapigo kwa kujibishana, kitu ambacho kilisababisha malumbano ambayo Aunt Ezekiel hakufurahishwa nayo na hivyo akaweka bandiko jipya ambalo lilisomeka kama ifuatavyo;

"Dini ni Imani ya Mtu toka Moyoni mwake plz Ukijua dini yako inatosha usilazimishe kujua na yawenzako Naheshimu na Kuamini Dini zote mbili usitake kujua zaidi Alhamdulilaah kwa yote Muwe na jumapili Njema dah!"

Jamani tukubali kila mtu na imani yake, hata kama hauipendi ya mwenzako, mheshumu basi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
20 Jan 2015

Post a Comment

 
Top