April 3, 2025 11:18:58 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mrembo na muigizaji wa filamu anayekuja kwa kasi, Ester Kiama amefunguka kuwa, wanaodhani ameingia kwenye fani ya uigizaji ili kutafuta wanaume wamebugi kwa kuwa yeye siyo mburula na hajui hata anaanzaanzaje kufanya hivyo.
Akizungumzia usumbufu anaoupata kutoka kwa vidume, Ester alisema wakati alipokuwa nje ya fani alikuwa hapati usumbufu lakini sasa ameamua kuonyesha kipaji chake anaonekana kama ameingia kujiuza kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wasiojitambua.
“Mimi bwana siyo mburula, nimeingia kwenye filamu ili kuonesha kipaji changu na wala si kuja kuuza sura wala kujiuza, wanaojiuza ni haohao, hivi mimi naanzaanzaje?” alisema Ester ambaye amefanya kweli kwenye filamu ya  Ngoma Ngumu inayotarajiwa kuingia mtaani wakati wowote.
GPL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
24 Jan 2015

Post a Comment

 
Top