
Klabu ya Chelsea baada ya kutupwa nje Kombe la FA leo imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Capital One baada ya kuifunga Liverpool bao 1-0 ikiwa katika dimba lake la nyumbani.
Bao la Chelsea limefungwa Dakika ya 94 (Katika muda wa ziada) na Branislav Ivanovic baada ya dakika 90 kumalizika milango yote ikiwa ni migumu.
Chelsea imefanikiwa kufuzu kwa jumla ya mabao 2-1 kutokana na matokeo ya sare ya bao 1-1 iliyoyapata katika mchezo wa Kwanza ikiwa ugenini, Anfield.
Chelsea sasa itasubiri mshindi kati ya Sheffield United na Tottenham Hotspur katika fainali ya kombe hili.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment