Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waziri wa Nishati na Madini mpya, George Simbachawene.
*****
Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo mchana, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Ombeni Sefue alitaja mawaziri hao wapya ambao wameapishwa leo jioni na wizara zao kwenye mabano kuwa ni: George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).

Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).

Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top