Tumuute Crying Beauty kwa picha hizi. Mrembo na shemeji/wifi yetu wa Uganda, Zari The Bosslady alijikuta akibubujikwa na machozi kutoka na na picha na maelezo aliyopewa kwenye jumba la makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, lililopo kwenye mji mkuu, Kigali.

Akiambatana na mchumba wake, Diamond Platnumz, Zari alishindwa kujizuia kulia kutokana na kumbukumbu ya kusikitisha ya mauaji hayo ya mwaka 1994 ambapo yapata watu 500,000–1,000,000 walipoteza maisha nchini humo.
“Everyone has a breaking point…. I was so touched,” aliandika mrembo huyo kwenye picha inayomuonesha akilia. “Women and children were raped then killed…. sad story. God bless you more Rwanda,” aliandika kwenye picha nyingine.


Mkono kwa mkono: Diamond na Zari wakiingia kwenye makumbusho ya mauaji hayo



Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment