Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MSANII wa filamu Bongo, Deogratius Shija hivi karibuni alizua timbwili baada ya kung’ang’ania kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye mtaa ambao siyo wake.
 
Msanii wa filamu Bongo, Deogratius Shija akizungumza jambo.
Chanzo makini kilieleza kwamba tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Mchangani, Mwananyamala, Dar ambapo wakala wa Chama cha CUF walimkatalia kwamba yeye siyo mkazi wa mtaa huo hivyo hapaswi kujiandikisha hapo ambapo Shija aliendelea kuzozana nao.
Paparazi wetu alimtafuta Shija ambapo alisema:


“Ni kweli nilienda kujiandikisha mawakala wakakataa nisijiandikishe kwa sababu nilishahama mtaa ambapo nilizozana nao hivyo baada ya vurugu kuzidi  polisi walikuja kuniondoa hata hivyo sikujiandikisha, kura sitapiga.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top