Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nick Minaj

Baada ya kutengana na mpenzi wake safaree Samuels,Hitmaker wa nyimbo ya Anaconda Nick Minaj ametaja vigezo vya mpenzi atakayekua naye kwa sasa.

Alisema moja ya vigezo anavyovitaka ni kupata mpenzi atakayekubali umahiri wake katika kazi zake na kuheshimu anachofanya.

“Nataka mwanaume atakayeheshimu na kuthamini uwezo wangu wa kufanya kazi.”alisema Nick Minaj.

Nick Minaj
Rapa huyo mwenye miaka 32 ameamua kuwa wazi baada ya kuvunjika kwa uhusiano wake na mpenzi wake Safaree uliodumu kwa miaka 12 na anahitaji umakini katika ufanyaji wake wa kazi.

Katika majibizano yake na mtangazaji Elliot Wilson alisema “Nimepoteza sehemu kubwa ya maisha yangu kwa kuachana na Safaree na sababu mojawapo nilikua busy zaidi na kazi ”

“Labda wanahitaji uangalizi zaidi na nilikua najali zaidi familia yangu,,sasa ni kazi yangu kuchagua kazi ama mapenzi.”alisema

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top