Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa sakafuni/kwenye korido kutokana na hospitali ya wilaya ya Mbogwe kukosa mochwari

Jeshi la polisi wilayani Mbogwe mkoani Geita linashikilia mwalimu wa shule ya msingi Kasandalala wilayani humo Laideth Constantine mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumnyonga mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 7 akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti).

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo 
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa geita Joseph Konyo amesema tayari wanamshikilia mtuhumiwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa mtoto huyo kanyongwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwalimu huyo amekuwa na mambo ya kushangaza jamii kwani wakati mwingine anajifanya mlokole,mara anakuwa mkali na kugombana na kila mtu hasa wakati akiwa shuleni.

“Tumekuwa tukimshangaa mwalimu huyu,kuna wakati anakuwa mlokole,wakati mwingine anakuwa,mtaratibu sana,sisi tunashangaa sana kutokea kwa tukio hili”,walisema.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Cosmas Kilosa amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa kunyongwa.

Credit:Malunde1 Blog

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top