
NI AIBU! Ndivyo unavyoweza kushangaa
baada ya mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kunywa pombe kiasi cha kupoteza fahamu akiwa na sare za
taasisi hiyo inayoheshimika nchini na kujikuta akilala karibu na mtaro,
katika stendi kuu ya mabasi mjini Iringa.
Anayedhaniwa kuwa mwananjeshi akiwa amelala kwenye mtaro.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema mtu
huyo alipanda basi liitwalo Mgumba huko Mafinga, ambako ipo kambi ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambalo lilikuwa likielekea mjini Iringa.
Abiria waliokuwa pamoja naye garini,
wanaripoti kuwa akiwa humo, tayari akionekana amelewa, aliendelea kunywa pombe kali inayokaa kwenye pakiti, maarufu kama viroba.
Akisimulia zaidi, mmoja wa abiria wa
basi hilo alisema akiwa bado anaendelea kunywa, ghafla alianza kutapika
na kujisaidia haja ndogo kiasi cha kuwachefua watu wengine.“Tulipofika
stendi, tukalazimika kumsaidia kumshusha huku akiwa hajitambui kabisa.
Akalala mtaroni, ikabidi tummwagie maji, ndipo alipozinduka na kupata
fahamu kidogo.
Baadhi ya watu wakimshangaa mwanajeshi huyo.
Alikuwa anaona aibu sana, akajikakamua
na kutoa namba ya simu ya rafiki yake, ambaye ni askari wa FFU mjini
Iringa, ambaye alipigiwa na kuja kumnusuru,” alisema abiria huyo
aliyekataa kutaja jina lake.
Gazeti hili liliwasiliana na kiongozi
mmoja wa kambi ya Jeshi Mafinga, ambaye baada ya kuelezwa kuhusu askari
huyo, alikiri kuwa ni mwenzao, lakini siyo wa kambi hiyo.
“Ni kweli nimeziona hizo picha, huyo
jamaa kweli ni askari mwenzetu lakini siyo wa kambi hii, huyo anatoka
Itende, Mbeya. Jaribu kuwasiliana nao kule wanaweza kukupatia taarifa
maana sisi tulishawataarifu,” alisema kiongozi huyo, aliyeomba hifadhi
ya jina lake kwa vile siyo msemaji wa Jeshi.
Juhudi za kumpata Mkuu wa Kikosi cha
Itende hazikuweza kufanikiwa, lakini Kaimu Msemaji wa Jeshi la Wananchi,
Makao Makuu Dar es Salaam, Meja Joseph Masanja, alipatikana na yeye
kukiri kuziona picha hizo mitandaoni.
“Ni kweli nimeziona picha hizo na ninazo
hapa, lakini kama unavyoziona, kuna gizagiza kiasi kwamba huwezi
kumtambua. Ni vigumu kusema huyo ni askari wetu kwa sababu picha
haionekani, huenda ni mtu tu kalewa akiwa na nguo za jeshi.
Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange.
Alipoulizwa kuhusu adhabu anayoweza
kupata endapo atafahamika kuwa ni mwanajeshi, Masanja alisema hayo ni
masuala ya utawala yanayotofautisha makosa ya kijinai na nidhamu.
“Vilevile inakuwa vigumu kidogo kujua
kwa nini mtu aliyepiga picha aliamua kuposti kwenye mitandao,” alisema
Meja Masanja akisisitiza Jeshi bado linaendelea kutafuta ukweli wa picha
hizo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment