Amou Haji Mzee wa zaidi ya miaka 75, Raia wa Iran, ndio Binadamu anayeshikiria rekodi ya kuwa Mwanaume mchafu zaidi duniani. Haji amekuwa na matatizo ya kisaikolojia kwa kujengewa imani tangu utotoni mwake kuwa, kitendo cha kusafisha mwili wake kitamsababishia maradhi.
Haji Hakubaliani kabisa na kunywa maji safi, na anachukia kabisa apoletewa habari za kuoga. Uchafu huu haujaishia tu kwenye usafi wa mwili wake, bali umeenda mbali zaidi kwa mzee huyu kuamua kuishi ndani ya shimo.
Chakula cha Haji ni Nyama zilizo oza lakini pia anatumia sigara zinazotengenezwa kwa vinyesi vya wanyama. Kitendo cha binadamu mchafu zaidi kuwa Mwanaume, kinafanya wanaume tuzidi kumulikwa zaidi kwenye swala la usafi wa miili yetu, mavazi na ushiriki wetu katika usafi wa mazingira.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment