Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mazishi Kny
Katika hali ya kushangaza familia moja ilijikuta katika hali ya furaha kwenye msiba, wakaimba na kucheza ngoma tofauti na ambavyo tumezoea kwamba msibani ni sehemu ambayo watu huwa na majonzi na huzuni.

Furaha hiyo ilitokana na kitendo cha Mahakama kuruhusu mazishi ya ndugu wa familia hiyo huko Kenya baada ya mwili wa marehemu huyo kukaa zaidi ya miaka mitano ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kutokana na kesi ya mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya marehemu na ndugu yake.
Ardhi ambayo ilikuwa ikigombaniwa ni sehemu ambapo alipaswa kuzikwa marehemu huyo, hivyo kutokana na kesi hiyo wakashindwa kufanya mazishi, wiki hii Mahakama kuu ya Nyeri iliruhusu mwili huo kuzikwa eneo hilo ambalo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu.
Kutoka kwenye taarifa iliyoripotiwa na Kituo cha K24, mwanakijiji mmoja alisema; “… sisi tulipanga mazishi, huyu kijana hakuweza kuzikwa kwa sababu huyu Mzee alienda kortini na kuweka ile mnaita ‘Court Injunction’ kwamba hawezi kuzikwa katika hili shamba, kwasababu iko na kesi na shamba ni yake kwa hiyo mtu hawezi kuzikwa katika hiyo shamba yake, hiyo ndiyo kesi imekuwa ikiendelea...
ndani

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top