Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wanajeshi wa AU wamekuwa wakipambana dhidi ya Al Shabaab na kuwafurusha kutoka Mogadihu
Jeshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa kundi la wanamgambo la al-Shabaab nchini Somalia.

Maafisa katika idara ya ulinzi wanasema kuwa wanajaribu kubaini ikiwa shambulizi hilo lilimuua mlengwa ambaye jina lake halijatajwa.
Shambulizi lililenga gari alimokuwa anasafiria mshukiwa huyo Kusini mwa Somalia karibu na mji wa Barawe.
Al-Shabab linasemekana kuwa na uhusiani na kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Taarifa kutoka katika makao makuu ya ulinzi nchini Marekani zinasema kuwa mlengwa katika shambulizi hilo ni kiongozi wa makundi mawili ya kigaidi.

Mmoja wa viongozi wa al shababaab anaseama kuwa mshukiwa alikuwa Sahal Iskudhuq, kamanda mmoja wa al-Shabaab ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu sana na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeeda.
Hata hivyo hakuna uhakika ikiwa mshukiwa huyo ameuawa.

Marekani iliwahi kufanya shambulizi ambalo lilitibuka dhidi ya mmoja wa viongozi wa kundi hilo katika eneo la Barawe - linalosemekana kuwa ngome kuu ya Al Shabaab mwezi Oktoba.

Al Shabaa waliohusika na mashambulizi ya kigaidi katika jengo la maduka la Westgate, limedhoofishwa na mapambano dhidi yao kutoka kwa wanajeshi wa Muungano wa Afrika
Kusini na Kati mwa Somalia. 


Marekani nayo imejitolea sana kukabiliana na kundi hilo kwa kutuma kikosi cha ushauri wa kijeshi mjini Mogadishu.
Source:bbcswahili

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top