Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mtuhumiwa wa wizi akiwa amechakazwa kwa kipigo. 
Moja ya matofali yaliyotumika kumshambulia mtuhumiwa.Wananchi wakiwa katika jaribio la kumvisha tairi na kumchoma moto.Mtuhumiwa akibebwa na askari.
Askari waliofika eneo la tukio.
Gari la polisi likiwa eneo la tukio.
Damu ikiwa imetapakaa eneo ‘alilosulubiwa’ mtuhumiwa.
Umati uliofurika kushuhudia tukio hilo.
Mtuhumiwa akiwa katika hali mbaya.
KIJANA ambaye jina lake haikufahamika mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa pikipiki jijini Dar.Tukio hilo la kusisimua limetokea asubuhi ya leo Magomeni-Mwembechai,  ambapo lilisababisha foleni ndefu ya  magari wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.
Mashuhuda wa tukio hili walisema kijana huyo na wenzake waliiba pikipiki mbali na hapo Mwembechai ila katika purukushani na wamiliki wa chombo kile, kijana yule alijikuta akianguka kutoka kwenye pikipiki eneo lile na kuzingirwa na waendesha pikipiki wa pale wanaojulikana kama ‘bodaboda’ walioanza kumshushia kipigo baada ya mmiliki wa pikipiki husika aliyekuwa akiwafukuza kusema kijana huyo alikuwa na wenzake waliokimbia na chombo hicho.
Pamoja na kipigo alichopewa, wananchi waliamua kumvisha tairi shingoni wakiwa tayari kumchoma moto ambapo dakika chache tu baadaye askari walifika na kumwokoa.
Kijana huyo aliyekuwa bado hai, aliokolewa na askari  wa doria waliomchukua pamoja na mtu aliyejitaja kama mmiliki wa pikipiki iliyoibiwa.
Picha na Global

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top