April 5, 2025 08:48:37 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


MTANGAZAJI  wa Redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amesema siku zote anapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi akigundua mtu wake ana ‘date’ na mwanamke mwingine, kamwe hatathubutu kugombea bwana ila atanawa mikono.

Mtangazaji wa Redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ akipozi.

Akibonga na paparazi wetu hivi karibuni Dida alisema, hakuna kitu ambacho kwake anaona ni cha kipuuzi kama kugombea penzi, kwa kuwa mtu anapokusaliti ni wazi upendo wake umehamia kwa mtu mwingine hivyo hawezi kujing’ang’aniza.

“Nawashangaa sana wasichana wanaokosa kazi ya kufanya kwa kuanza kuwagombea wanaume, wengine wanadundana hadi kutoana manundu, hivi nigombee bwana kwani wanaume wameisha?  Mimi nikimkuta mtu wangu yupo na mtu mwingine wala sijishughulishi, nachukua hamsini zangu,” alisema Dida.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
12 Dec 2014

Post a Comment

 
Top