Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wachezaji wa timu ya England wakishangilia baada ya mechi yao dhidi ya Scotland kumalizika. Katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa usiku wa kuamkia leo, England walishinda kwa mabao 3-1.
Alex Oxlade-Chamberlain akifunga bao la kwanza kwa England dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Kapteni wa Scotland, Scott Brown (kushoto) na wa England, Wayne Rooney (kulia) wakisalimiana kabla ya mechi.
Wayne Rooney akipongezwa na Danny Welbeck (wa pili kulia) na Chris Smalling (kushoto).

Mshambuliaji wa timu ya England, Danny Welbeck (katikati) akiwania mpira na Russell Martin (kulia).
Rooney akishangilia baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 85 kipindi cha pili.
Wilshere (kulia) akiwatoka wachezaji wa Scotland.
ENGLAND imewalaza wenyeji Scotland mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku wa kuamkia leo.
Wafungaji wa mabao ya England, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 32 na Wayne Rooney aliyefunga mabao mawili dakika za 47 na 85, wakati bao pekee la wenyeji lilifungwa na Andrew Robertson dakika ya 83.
Scotland: Marshall/Gordon dk 46, Whittaker, R Martin, Hanley/May dk 66, Robertson, Maloney, Mulgrew, Brown/D Fletcher dk 46, Anya/Bannan dk 61, C Martin/Morrison dk 46 na Naismith.
England: Forster, Clyne, Cahill/Jagielka dk 46, Smalling, Shaw/Gibbs dk 66, Oxlade-Chamberlain, Milner, Wilshere/Barkley dk 87, Downing/Lallana dk 46, Rooney na Welbeck/Sterling dk 46.
Matokeo mengine
FT     Japan     2 - 1     Australia
FT     Thailand     2 - 0     New Zealand
FT     China     0 - 0     Honduras
FT     Iran     1 - 0     South Korea
FT     Slovakia     2 - 1     Finland
FT     Belarus     3 - 2     Mexico
FT     Greece     0 - 2     Serbia
FT     Slovenia     0 - 1     Colombia
FT     Austria     1 - 2     Brazil
FT     Estonia     1 - 0     Jordan
FT     Romania     2 - 0     Denmark
FT     Ukraine     0 - 0     Lithuania
FT     Hungary     1 - 2     Russia
FT     Ireland     4 - 1     USA
FT     Italy     1 - 0     Albania
FT     Poland     2 - 2     Switzerland
FT     Portugal     1 - 0     Argentina
FT     Spain     0 - 1     Germany
FT     France     1 - 0     Sweden

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top