Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha
katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)
Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa
Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.
Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA
aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni
40.4
Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri
wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4
Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la
Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4
Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi
ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip
Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9
Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa
milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.
Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.
Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4
Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.
Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha
NA HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA KAMATI
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWAJIBISHWE KWA
KUUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA - MAPENDEKEZO YA
KAMATI YA ZITTO
Filikunjombe: Kamati inashauri kuzitangaza benki za
Stanbic na Mkombozi kama asasi za utakatishaji fedha
Filikunjombe: Kamati inashauri bodi ya Tanesco ivunjwe na
TAKUKURU iwafungulie mashtaka ya rushwa.
Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Naibu waziri wa
nishati na madini alisema uongo bungeni naye achukuliwe
hatua.
Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa
Nishati na Madini Sospeter Muhongo amekuwa akisema
uongo mara nyingi.
Filikunjombe: Kamati pia imethibitisha kuwa Waziri
wa nishati na madini ndiye alikuwa dalali mkuu wa
kuunganisha hawa watu
Filikunjombe: Kutokana na sababu hizo hapo juu, kamati
inapendekeza kuwa Waziri wa Nishati na madini
avuliwe madaraka yake.
Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa mwanasheria
mkuu wa serikali utengeuliwe mara moja na
aadhibishwe maana ametumia vibaya madaraka
Filikunjombe: Kamati pasipo mashaka imejidhihirisha kuwa
Waziri mkuu alikuwa akijua jambo hili ila hakuchukua
tahadhari.
Filikunjombe: alisema Mwalimu Nyerere kuwa kumbadili
Waziri Mkuu sio jambo la ajabu.
Kwa vyovyote vile, Waziri mkuu anapaswa kuwajibishwa
kwa namna yoyote ile ili kurudisha heshima ya
serikali maana ameudanganya umma wa Watanzania kwa
kusema uongo na kuitete kampuni hewa ya PAP isiyokuwepo
Filikunjombe: Kamati yetu inaamini kuwa Bunge hili
litaitumia vizuri taarifa yetu hii
Mh. Spika anna Makinda amehairisha shughuli za Bunge na
kusema kuwa kesho asubuhi serikali itatoa kauli zake.
Baada ya serikali kutoa kauli zake hapo kesho asubuhi, Wabunge wengine watapata nafasi ya kuchangia.
Credit Jamiiforums.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro












.jpg)


Post a Comment
Post a Comment