Mtoto aitwaye Paschal Bundala mwenye umri wa miaka 7 mkazi wa kata ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha, tukio hilo limetokea Novemba 15 mwaka huu wakati mtoto huyo akichunga Ng’ombe.
Hata hivyo Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha tukio hilo ni mtoto huyo kuteleza na kutumbukia kwenye dimbwi hilo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment