Wagonjwa waliolazwa na kupata matibabu katika kituo cha Afya Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera, juzi wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kupata kipigo kutoka kwa mganga wa
kituo hicho ambaye aliwataka kushiriki zoezi la usafi katika vyumba na mazingira ya kituo hicho.
kituo hicho ambaye aliwataka kushiriki zoezi la usafi katika vyumba na mazingira ya kituo hicho.
Wakizungumza na wanahabari kituoni hapo, wagonjwa hao walidai kuwa
Mganga Mkuu wa kituo hicho, Fred Nyangosie aliwapiga wagonjwa na jamaa zao akiwataka wafanye usafi, huku wengine wakiwa ni wagonjwa wasiojiweza.
Mmoja wa wagonjwa hao, Ester Bonifasi aliyekuwa akipata matibabu katika kituohicho, alisema kituoni hapo kuna utaratibu wa kuzuia wagonjwa kulia chakula wodini, hivyo walipokutwa wakikiuka utaratibu huo walianza kupigwa na mganga huyo.
Alisema mganga na wafanyakazi walianza kuwaburuta waliokuwa ndani ya wodi zawagonjwa na kuamriwa kufanya usafi, huku waliokuwa wakizubaa kutafuta zana za kufanyia usafi huo, walikuwa wakipigwa na watu kukimbia ovyo.
Aidha kijana Samweli Gwassa alisema yeye alikamatwa na mganga huyo nakumfungia kwenye chumba maalumu kilichojulikana kuwa ni mahabusu alipokuwa akiegesha baiskeli yake pembeni ili akachukue kwanja.
Mganga Mkuu wa kituo hicho, Fred Nyangosie hakutaka kutoa maelezo ya chanzo cha kuwapiga wagonjwa na jamaa zao bali alidai kuwa ili aweze kuongea lazima awe na kibali kutoka kwa mwajiri wake.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Colnery Ngudungialisema Kamati ya Afya ya Wilaya itakaa na kujadili changamoto za kituo hicho nauamuzi utakaotolewa atawajulisha wananchi na utoaji huduma unaendelea.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment