Idadi ya raia wa Nigeria wanaokamatwa na dawa za kulevya inazidi kupanda siku hadi siku, ambapo taarifa iliyopo ni kwamba mtu mmoja mwenye umri wa miaka 35 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
Jamaa huyo Abuchi Ngwoke alikamatwa mwaka 2012 uwanja wa ndege wa Malaysia baada ya kukamatwa na dawa hizo zenye uzito wa gramu 251.66 aina ya Methamphetamine ambazo alikuwa akisafirisha kutoka Nigeria kwenda Malaysia.
Ni mara nyingi tumekuwa tukisikia kuhusu watu wanaokamatwa kwa kusafirisha dawa hizo huku wengi wao wakitajwa kuwa ni Wanigeria.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment