Hali kwenye klabu ya Liverpool imeendelea kuwa mbaya baada ya kupoteza mchezo wake wa tatu mfululizo kwenye ligi ya England .
Liverpool iliuona uwanja wa Selhurst Park mchungu baada ya kufungwa 3-1 kwenye mchezo wao dhidi ya Crystal Palace .
Wekundu hao wa huko Anfield walianza kufunga kupitia kwa Ricky Lambert ambaye alikuwa anafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool akitokea Southampton .
Hata hivyo Crystal Palace ilirudisha mabao hayo kupitia kwa Mile Jedinak , Dwight Gayle na Joe Ledley.
Matokeo haya yanaifanya Liverpool ibaki kwenye nafasi ya 12 baada ya kupoteza michezo 6 kati ya 12 ya msimu huu kwenye ligi ya England .
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment