
Wabunge wa upinzani wakiondoka bungeni Dodoma jana usiku baada ya kikao cha Bunge hilo kuvunjika. Picha na Emmanuel Herman
Dar/Dodoma. Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku kilivunjika baada ya vurugu kutawala ukumbini humo.
Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge hadi leo saa tatu asubuhi.
Chanzo cha vurugu ni kutokana na ugumu wa kutokukubaliana na azimio la tisa, lililolenga kumwajibisha moja kwa moja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Azimio la PAC lilitaka Waziri Muhongo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma zilizokuwa zinazomkabili ikiwamo kulidanganya Bunge.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengi wakiwa wa CCM walitaka waziri huyo asiadhibiwe na Bunge bali achukuliwe hatua na mamlaka iliyomteua.
Wakati ubishani huo ukiendelea, ikiwa imefika saa 4.42 usiku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama na Spika Makinda alimruhusu kuzungumza.
“Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo (jana) kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi,” ilikuwa ni kauli ya Mbowe.
Mara baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge wote wa upinzani walisimama na kuanza kupiga kelele kwamba wezi waondoke…tunataka fedha zirudi…tunataka fedha zirudi…vijana msilale…vijana msilale.
Wakati wabunge hao wakiendelea kuimba, wabunge wa CCM wao walikuwa wakizunguka zunguka huku wengine wakitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Hata hivyo, wabunge wa upinzani waliendelea kusimama, kuimba na kupiga makofi, huku wabunge wa CCM wakimpongeza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuruka kihunzi alichokuwa amewekewa na kamati ya PAC.soama zaidi hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment