Stori: Hamida hassan na Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula (pichani) maarufu kama Johari, hivi karibuni alidaiwa kuonekana akiingia nyumbani kwa mganga wa kienyeji (jina linahifadhiwa) katika Kijiji cha Kibeta, mjini Bukoba mkoani Kagera.
Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa Johari akiwa katika bodaboda, aliingia kwa mganga huyo wa kike anayefahamika sana eneo hilo.
“Sijui nilikuwa namfananisha? Nimemuona msanii wenu hapa Kibeta akiingia kwa mganga ila nimeshindwa kumpiga picha maana kasimu kangu ni ka’ tochi, labda kaja kuweka mambo yake sawa,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizi, mwandishi wetu fasta alibonyeza namba za Johari katika simu yake ambaye alikiri kuwepo Bukoba kwa siku mbili kwa shughuli zake.
“Jamani siyo kila kitu muandike, mmejuaje mimi nilienda Bukoba, naomba hii isiwe habari tafadhali si ulimwengu mzima ujue mimi nimefanya nini,” alisema Johari, mmoja wa waigizaji nyota na mkurugenzi mwenza wa RJ Company.
Katika kujitetea zaidi, Johari alisema alikwenda Bukoba kwa mama yake mkubwa, (jina linahifadhiwa) ambaye hakujua kama anajishughulisha na mambo ya uganga kwani hakuwahi kusikia.
“Sikupenda hii habari kabisa, lakini kiukweli nilienda kumuona mama yangu mkubwa nikiwa na ndugu zangu wengine, kwani alikuwa akiumwa, sikukaa sana, nilikaa siku mbili tu na kugeuza kwani nilikuwa nikitokea Shinyanga kwenye msiba kama ulisikia nilifiwa,” alisema na kuongeza kuwa hajawahi kupanda pikipiki kwani magari yapo tena kwa bei rahisi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- VIDEO: Mama Wema Aeleza Beef yake na Man Fongo Kisa……..09 Sep 20160
NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa ...Read more ?
- Busu la Nelly Kamwelu shavuni kwa Diamond akiwa na Wizkid lawatoa povu mashabiki (Video)25 Aug 20160
Haipiti wiki bila Diamond kuwatoa povu mashabiki, hata kama alichokifanya si kwamba alidhamiria...Read more ?
- Picha za Masanja na Mke wake Zazua Maswali Kwa Mashabiki wake..Wadai Mke wa Mchungaji Apaswi Kuvaa Hivyo19 Aug 20160
Baada ya Harusi ya Mchekeshaji Masanja na Mkewe iliyofungwa Jumapili iliyopita wawili hao wameon...Read more ?
- AUDIO: Kitu Diamond kasema kuhusu yeye kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto03 Aug 20160
Ukaribu wako kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori...Read more ?
- Shamsa Ford Amuweka Wazi Mpenzi wake Mpya03 Aug 20160
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa baada ya kuachana na mpenzi wake wa...Read more ?
- Madai: Flora Amwangukia Mbasha30 Jul 20160
Habari ya mjini ni Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha kudaiwa kumwangukia mumewe waliyetengana, Em...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment