Taarifa kuhusiana na hali ya kiafya ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye yupo Maryland Marekani kwa ajili ya matibabu, imesema hali yake kiafya inaimarika na ameanza mazoezi ya kutembea ikiwa ni siku ya pili tangu afanyiwe upasuaji wa tezi dume.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtoto wa Rais Kikwete, Miraj Kikwete (@kikwete) ameweka picha muda mfupi uliopita inayomwonyesha Rais pamoja na maneno haya;- “… #26464 #we #good TABASAMU TU LEO . thank you everyone for your endless support, love and prayers. It means so much to Dad, myself and our family. You are a strength to us. TUNAWASHUKURU KWA KUJALI ….“

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment