GOOD news kwa mtoto mzuri
Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ni kwamba anatarajia kuolewa hivi
karibuni baada ya kuishi maisha ya upweke kwa muda mrefu, Risasi
Jumamosi linakujuza.
Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili, ameliambia Risasi Jumamosi
kuwa kwa umri alionao, amejifunza vitu vingi katika maisha hivyo kwa
kuwa ameshampata mtu sahihi kwake, ameona bora aolewe.
Alisema katika safari ya maisha, vikwazo ni vingi ikiwemo masuala ya
skendo za wasanii lakini ameshavuka vikwazo hivyo na hahitaji tena
kuyumbishwa na mtu kwani anaingia kwenye ndoa akiwa ameshajifunza mengi.
“Ndoa siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi
wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu tunakutana katika mazingira mbalimbali
hatarishi na wadau tofauti, vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi
ni jambo la kumshukuru Mungu,” alisema Batuli.
Paparazi wetu alimbana zaidi Batuli ili aweze kujua hiyo ‘hivi
karibuni’ kwake ina maana ya lini ambapo hakutaka kutaja tarehe ya
harusi lakini akaahidi kumwanika mume wake mtarajiwa Desemba 5, mwaka
huu sambamba na kutaja siku husika ya ndoa.
“Wewe usijali, utakuwa wa kwanza kualikwa. Tena Desemba 5 nitakuita
umuone mume wangu mtarajiwa, nitakutambulisha kwa majina na kila kitu,
baada ya hapo nitakupa tarehe kamili ya ndoa yangu maana kila kitu
kimeshakaa kwenye mstari, soon tu nitakuwa mke wa mtu,” alisema Batuli.
Watoto wawili ambao Batuli anao kwa sasa, alizaa na wanaume wawili
tofauti ambao hapendi kuwazungumzia kwa kuwa tayari zama zao
zilishapita.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment