Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
My confession! (kukiri kwangu)! Mwanadada mwenye taito ya utangazaji na uigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefungua kinywa na kutoa la moyoni akisimulia tukio baya lililowahi kumkuta la jinsi alivyobakwa, Risasi Jumamosi lina ‘exclusive story’.
TUJIUNGE DUKANI KWAKE
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni dukani kwake Kinondoni jijini Dar, Aunty Lulu asiyeishiwa na vimbwanga alisema kwamba, kamwe hawezi kusahau tukio hilo maishani mwake.
ALIBAKWA NA RAFIKI WA SHEMEJI YAKE
Aunty Lulu aliyeng’ara kwenye Sinema ya Lost Soul alieleza namna alivyobakwa na rafiki wa shemeji yake (rafiki wa mume wa dada yake) na kumpotezea ndoto zake za kuanza mchezo huo akiwa ndani ya ndoa.
Akieleza kwa uchungu na masikitiko, Aunty Lulu alitiririka kwamba, alikuwa akiishi kwa dada yake ambapo rafiki wa mume wa dada yake huyo alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani kila wakati alipokuwa akifanya kazi maeneo ya Posta jijini Dar.
KISUTU SEKONDARI
Aunt Lulu alisema kwamba wakati huo, yeye alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Kisutu, Dar, hivyo kila siku jioni mwanaume huyo alikuwa akimpitia na kumpa lifti hadi nyumbani.
Aliendelea kusema kwamba, siku moja jamaa huyo aliyekuwa amemzidi umri maradufu alimtaka wafanye mapenzi lakini alimkatalia kwa madai kwamba hakuwahi kufanya mchezo huo mbaya ambao alifundishwa kuwa ni dhambi.
TUKIO BLOCK 41
“Kwa kawaida yule jamaa alikuwa akinifikisha nyumbani kwa dada yangu pale Makumbusho (Dar), ananisubiri, nabadilisha nguo, naenda naye kwake maeneo ya Block 41 (Kinondoni) ambako alikuwa akinifundisha. So alinibakia nyumbani kwake,” alisema Aunty Lulu, mtangazaji wa zamani wa ITV na C2C.
MAUMIVU MAKALI
Staa huyo aliendelea kutiririka kwamba alipomwambia kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho, mwanaume huyo alimwambia haamini ndipo akamkamata kinguvu na kumpeleka chumbani kwake kisha akamwingilia na kumsababishia maumivu makali. “Kwa kuwa niliumia sana, nilikuwa natembea kwa shida hivyo dada yangu aligundua.
AGOMA KUTAJA MWANAUME
“Ilibidi dada anibane kujua nina tatizo gani. Kwa kuwa nilikuwa sina ujanja nilimwambia nimeingiliwa kwa mara ya kwanza lakini nilisita kumtaja mwanaume huyo.
“Dada aliponibana sana nilimwambia kwamba niliingiliwa na huyo rafiki wa mume wake.
INASIKITISHA
“Lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana na ukweli liliwaumiza sana dada na shemeji yangu.
“Walimsema sana mwanaume huyo na ikawa ndiyo mwisho wa urafiki wao.
ALIKUWA NA UMRI GANI?
“Umri sikumbuki lakini nakumbuka nilikuwa nakaribia kuingia kidato cha nne. Yule mwanaume alizoea kuninunulia vifaa vya shule na kunisisitiza kusoma.
“Nilimuona mtu bora sana, nikamzoea na ikawa rahisi kwenda kwake kusoma maana jamaa alikuwa ‘jiniazi’ na mwanzoni alikuwa jirani yetu kabla ya kuhama.
“Ukweli huwa sipendi kuelezea historia ya maisha yangu ya mapenzi kwani inaniumiza sana.
AMPOTEZEA NDOTO YA KUOLEWA
“Huwa najisikia kulia kwa sababu huyo rafiki wa shemeji yangu alinipotezea ndoto nilizokuwa nazo kwamba nitafanya juu chini niolewe nikiwa ‘mbichi’ hivyo mapenzi ningefanya nikiwa ndani ya ndoa.
“Sikufurahia kabisa kitendo hicho maana naona pia kiliniathiri kisaikolojia,” alisema Aunty Lulu.
YUPO WAPI MWANAUME HUYO?
“Baada ya tukio lile aliomba anioe ili nimsamehe lakini nilikataa. Baadaye alikwenda kusoma nje ndipo tukapotezana na sijawahi kumuona tena, nasimulia ili liwe fundisho kwa wanawake wanaopenda kuwa na ukaribu kupitiliza na wanaume wasiowajua kiundani,” aliweka nukta Aunty Lulu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Diamond kuwania tuzo 5 za Afrima 2016, Alikiba na Yamoto Band moja08 Sep 20160
Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele vitano kwenye tuzo za mwaka huu za Afrima. Vipeng...Read more ?
- Ujumbe wa Diamond kwa bintiye Wazua Gumzo......Kamwambia "Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana"23 Jul 20160
Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii. Lakini ujumbe wake mpya...Read more ?
- Bifu Kali Kati ya Diamond na Clouds Media23 May 20160
Ni dhahiri sasa msanii wa kimataifa Diamond na brand kubwa ya radio na tv Clouds Fm, bifu la hadh...Read more ?
- Afande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi02 Feb 20160
Msanii mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na kusema serikali ihalalishe matumiz...Read more ?
- Gari Jipya Analomiliki Masanja Mkandamizaji.10 Jan 20160
Msanii wa Vichekesho Anawakilisha kundi la Orijino Komedi anayejulikana kama Masanja Mkand...Read more ?
- Zari The Lady Boss Awakosha Mashabiki wa Penzi lake na Diamond Kwa Picha Hizi09 Jan 20160
Zari the Boss Lady ‘Mama Tiffah’ amewakosha mashabiki wa penzi lake na Diamond ‘Baba Tiffah’ baada...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment