Vijana wawili wakazi wa kata ya Sombetini jijini Arusha wamefariki dunia baada ya chumba walichokuwa wamelala kikiwa kimejengwa kwa mabanzi kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia November 28 /2014.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kamshna msaidizi Edward Balele amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo cha moto ulipekelea vifo vya vijana hao Bw, Mohamed Katendela Juma na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Agaste ni mshumaa waliokuwa wanautumia kama nishati kwenye kibanda chao.

Kaimu kamanda Balele ameongeza kuwa pia uchunguzi unaonyesha kuwa marehemu walikuwa na kawaida ya kutumia kilevi kupita kiasi maelezo ambayo yamethibitishwa na baadhi ya majirani.
Wapangaji wa nyumba kilipojengwa kibanda hicho kilichoungua wamesema kuwa vijana hao watoka kila siku asubuhi kwenda kwenye shughuli zao na kurudi jioni na mmliki wa nyumba na kibanda hicho ambacho hakina umeme Bi Sioni Leomoni amesema pia wana kawaida ya kupika na kuvuta sigara ndani ya kibadna hicho.
Diwani wa kata ya Sombetini Bw Aally Bananga amesema pamoja na ukweli kuwa ajali haina kinga lakini kuna haja ya kila mmoja kutimiza wajibu wake wa kuchukua tahadhari juu ya mambo yanayoweza kuhatarisha maisha yake na ya wengine.
CDT...ITV
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment