Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This




Mtu mmoja anasemekana kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa baada ya Magari Mawili waliyokuwa wanaendesha kugongana uso kwa uso katika eneo la Trans Oil kata ya Nyasubi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo.
 

Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku jana likihusisha gari aina ya Coster mali ya Kampuni ya CK Safari Tours yenye namba T-468-CAL kugongana na Semi Teller aina ya Scania yenye namba T-498-BVH.

Kwa mujibu wa Mashuhuda, gari aina ya Coster ilikuwa ikitokea eneo la kituo cha Mafuta kwenda Phantom, huku Scania hiyo ikitokea jijini Dar-es-salaam kwenda nchi jirani na ndipo zikagongana uso kwa uso.
Taarifa zinasema Dereva wa Scania hiyo ndiye huenda amefariki dunia huku dereva wa Coster hiyo akisemekana kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu.



Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na tayari Jeshi la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na taratibu za kuyatoa magari hayo katikati ya barabara zinaendelea.
Bonyeza Hapa kuungana nasi facebook

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top