Rais wa shirikisho la soka barani afrika Issa Hayatou
Kulingana na shirikisho la soka barani Afrika, taifa hilo limetajwa baada ya Morrocco kukataa kuandaa michezo hiyo kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Morrocco ilikuwa imeiomba CAF kuahirisha dimba hilo la January 17 hadi Feruary 8.
CAF vilevile imeipiga marufuku Morrocco kushiriki katika dimba hilo ambalo sasa litaandaliwa na taifa lililoandaa kombe hilo na Gabon mwaka 2012.Kombe la michuano ya bara Afrika
Equitorial Guinea sasa itachukua jukumu lote la kuandaa michuano hiyo yenye mataifa 16.
CAF imetangaza kuwa mechi hizo zitachezwa katika miji minne ikiwemo Malabo,Mongomo na Ebebiyin.Droo ya mechi hizo itafanyika mjini Malabo tarahe 3 mwezi Disemba.
Haijabainika iwapo mwenyeji huyo mpya atashiriki katika dimba hilo kwa kuwa timu hiyo ilipigwa marufuku mwezi Julai kwa kuchezesha mchezaji asiyetakikana katika mechi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya Mauritania mnamo mwezi May 17.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment