July 31, 2025 09:49:13 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Gloves IIUnapokuwa mwamuzi wa mchezo fulani, ni muhimu basi uwe na ujuzi wa kutosha pia katika kuumudu mchezo husika japo kidogo,  hii ninayokuletea sasa hivi huenda ikawa ngeni sana kuwahi kuiona ama kuisikia mtu wangu.
Mwamuzi wa mchezo wa masumbwi Mageja Dziurgota amepelekwa hospitalini huko Croatia kupata matibabu baada ya kujikuta akishushiwa makonde ya kutosha na bondia Vido Loncar (18) aliyekuwa akipambana na bondia kutoka Lithuania, Algirdas Baniulis.

Janga hilo la mwaka limemkuta mwamuzi huyo mara baada ya kumtangaza Baniulis kuwa mshindi katika pambano hilo.
Shirikisho la mchezo wa masumbwi limemfungia bondia huyo kucheza pambano lolote, japo wanaamini kuwa bondia huyo si ‘mnyama’ kama anavyodhaniwa na watu baada ya kumtwanga makonde mwamuzi huyo.
Video iliyopo katika mtandao wa Youtube inayoonesha tukio zima la mkasa huo, imepata watazamaji zaidi ya milioni 2 ndani ya masaa 40, kwako mtu wa nguvu nafasi yako kuitazama pia.

Kama kifaa chako hakina uwezo Bonyeza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
22 Oct 2014

Post a Comment

 
Top