
ITV wameripoti kuhusiana na tukio hilo, ambapo moto huo umezuka ghafla wakati wanafunzi wakiwa katika ibada na hata baada ya taarifa kuwafikia askari wa kikosi cha zimamoto hawakutoa ushirikiano wowote kwa madai kuwa magari ya kuzima moto ni mabovu kitendo kilichowasikitisha mkuu wa shule hiyo Simon Kyala pamoja na askofu wa kanisa hilo Mhashamu Elias Chakupewa.
Thamani ya vitu vilivyoteketea bado haijafahamika japo mkuu wa shule amekiri kuwa wanafunzi hao wameathiriwa na janga hilo kipindi ambacho wanakaribia kuanza mitihani.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment