Kufuatia
tukio la Diamond Platinumz kuonekana akiperform na sare zinazoaminika
kuwa za jeshi la Wananchi (JWTZ), imeelezwa kuwa jeshi la Polisi
limemshikilia meneja wa Diamond, Babu Tale na inaelezwa kuwa alilala
selo.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa katika eneo la kituo cha polisi cha
Osterbay, Dar es Salaam jana (October 21), Babu Tale alifikishwa katika
kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi na polisi walionekana katika
eneo hilo.
Chanzo
hicho kimeeleza kuwa Uongozi wa Diamond ulipewa muda wa kujieleza kabla
ya saa mbili asubuhi, October 21 lakini haukufanya hivyo na ndipo hatua
hiyo ikachukuliwa.
Haijafahamika
bado kwa nini jeshi la Polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila
Diamond lakini vyanzo vimeeleza kuwa mwanamuziki huyo yuko safarini.
Hadi habari hii inaenda hewani, namba ya simu ya Babu Tale ilikuwa haipatikani.
Tovuti
ya Times Fm imeongea na kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa
Kinondoni, Dar es Salaam, Camillus Wambura ambaye amesema bado
hajawasiliana na kituo cha Osterbay kuhusu suala hilo na hajapata
taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya mkuu wa
upelelezi wa Mkoa.
“Mimi
ninachojua kuwa suala hilo liko chini ya uchunguzi. Habari ya
kushikiliwa watu na nini bado sijafahamu. Najua tu suala hilo liko
chini ya uchunguzi na linafanyiwa uchunguzi. Hiyo ni kesi ambayo iko
chini ya mkuu wa upelelezi wa Wilaya, chini ya mkuu wa upelelezi wa
Mkoa. Kwa hiyo sijapokea taarifa ya uchunguzi huo ulipofika.” Ameiambia
tovuti ya Times Fm.
Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
“Uchunguzi
unafanywa huko. Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi sana.
Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa
Mkoa. Kwa hiyo sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi
wa suala hilo,”ameongeza kamanda Wambura.
Mapema wiki hii, jeshi la wananchi Tanzania lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
chanzo:timesfm
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment