Kama mambo yangeenda yalivyokuwa yamepangwa, baada ya Ramadhan, Wema Sepetu angekuwa akiitwa Wema Naseeb! Lakini kutokana na sababu mbalimbali Diamond Platnumz alisogeza mbele mipango ya kufunga ndoa na mpenzi wake huyo.

Katika hatua nyingine, Diamond alisema hajamtenga baba yake kama inavyoandikwa kwenye magazeti ya udaku.
“Mzee Abdul sina matatizo naye baba yangu, bahati mbaya sikubahatika kukaa naye sana,” alisema Diamond. “Sometimes naendaga kwao sio mara kwa mara. Unajua vingi vya uongo na wanaandika vingi, sema sikubahatika kukaa na baba yangu sana ndio maana sikuweza kujua yeye na mama yangu wana matatizo gani”
“Sasa inakuwa ni ngumu kwa sababu nimeshamzoea mama yangu. Sema kwa sasa nina muda sana sijaonana naye kiukweli na muda mrefu sijaenda na nini. Lakini kila siku nikikaa na mama yangu ananiambia ‘msamehe yule ni baba yako’ Sometimes anadhani mimi bado nina kinyongo. Mama yangu ni mtu ambaye ananisihi sana ananiambia ‘nenda kwa baba yako usifanye hivyo kama vitu vilitokea na vimeshapita’,’ Nimeshamsemehe.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment