MAHABAT! Kuonesha kwamba mahaba yamemkolea, staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ amedaiwa kukacha shughuli za muziki na kutumikia penzi lake kwa mahaba motomoto.

Staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ akiwa na mwandani wake, DJ Hunter.
Kudhihirisha hilo, chanzo chetu kimevujisha picha za mrembo huyo akiwa na mchumba wake anayefahamika kwa jina moja la DJ Hunter wakiwa katika malovee mazito kwa kupigana mabusu.

Meneja wa Snura, Mohamed Kavu ‘HK’.
Jitihada za kumpata msanii huyo kuzungumzia ukimya wake kwenye gemu hazikuzaa matunda lakini meneja wake, Mohamed Kavu ‘HK’ amekuwa akisisitiza kuwa msanii wake huyo yupo nchini Afrika Kusini katika shughuli za kimuziki huku pia kukiwa na madai kuwa msanii huyo ni mjamzito tarifa ambazo pia zinakanusha na HK.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment