Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
q_chillar - bongoclan.co.tz

Mapya yanazidi kuibuka kuhusu ushindani wa Diamond na Ali Kiba amba ulianzia katika hitimisho la tamasha la Fiesta lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club Dar. Mashabiki wa wasanii hawa wawili wanavutana huku kila mmoja akisema mwenzake ana kipaji na anamfunika mwenzake. Inasemekana kua kuna baadhi ya mashabiki walikodiwa kwa ajili ya kumzomea Diamond wakati akitoa burudani siku ya Fiesta na hilo lilithibitishwa na Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond.
Tumepata bahati ya kufanya mahojiano na Q Chief na haya ndio mahojiano yetu na Q Chief
Mwandishi : kwa sasa katika mziki wa BongoFlava kumekua kuna fitini nyingi wakati mwingine wasanii kwa wasanii wanachonganishwa na mwisho wa siku unakua ugomvi, kwa mfano sasa hivi bifu la Ali Kiba na Diamond. Je Q Chie unalizungumziaje hili?
Q Chief : Yote wanayopitia ni changamoto ambazo pengine hawakuwahi kuzania kwamba watapitia. Mi nmepitia situation ambazo zimenijenga kua sugu na Legendary ndio maana ya kua mkongwe unapitia situation ambazo watu wengine wanakufosi ufike huko. Hata kama upo level fulani wanakushusha kwa kufikiria kwamba wanaweza kukushusha. unapandishwa na watu, unapandishwa na mwenyezi Mungu, unashushwa na watu, unashushwa na mwenyezi Mungu. Mfano nimekua nikiangalia Fiesta kwenye TV sikwenda kwa sababu nlikua na mambo yangu Studio, hakuna kitu kigeni nlichokiona, nmeona msanii wa marekani anafunikwa na msanii wa Tanzania ambaye ni Ali Kiba. Nmeona Ali Kiba ambaye amekaa kimya kwa miaka mitatu bila Airtime na watu wamemzungumzia vibaya, vizuri na nini wamemkubali tena. Ikiwa ni mtu yule yule ambaye wamemkataa na wakumuweka mtu mwingine juu. Hakuna kitu kisichowezekana, matokeo uliyoyaona juzi ndio matokeo yanayotokea na yataendelea kutokea. Hakuna Mungu wa hii kazi, hakunaga mfalme wa hii kazi ila kuna masultan wa Hii Kazi.

Unaweza msikiliza zaidi Q Chief hapa chini……
Source Bongoclan na Sweetbert wa Zenji Fm

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top