Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamume mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kutumia udanganyifu na kujidai kuwa mgonjwa mahututi kwa miaka miwili nchini Uingereza ili kukwepa mkono wa sheria.141023095019_mhalifu_ajidai_512x288_bbc_nocredit
Mwanamume huyo kwa jina Alan Knight, mwenye umri wa miaka 47, kutoka mtaa wa Swansea,aliamua kujidai kuwa mgonjwa baada ya kushtakiwa na polisi kwa kosa la kumuibia mzee mmoja jirani yake pauni elfu arobaini.
Pindi alipogundua kuwa alikuwa anasakwa na polisi, Knight alikwenda hospitalini kwa kutumia kiti cha magurudumu akiwa anatumia gesi ya Oxygen na kudangaya kuwa hawezi kutembea kutokana na kupooza kutoka shingoni hadi miguuni.
Kila wakati polisi walipotaka kumfikisha mahakamani , Knight alipelekwa na mkewe hositalini akidai kuwa amezidiwa.


Hata hivyo siku zake za mwizi kushikwa zilifika pale wauguzi walipompata katika chumba chake hospitalini akiwa anakula , kupanguza mdomo wake na hata kuandika.141023095720_mke_mhalifu_512x288_bbc_nocredit
Kwa miaka miwili, Knight alikwepa mkono wa sheria kwa kudai kuwa alikuwa hawezi kuamka wala kutembea na pia alikuwa tayari na uraibu wa kutumia gesi ya oxygen kama mtu ambaye hawezi kupumua bila usaidizi wa gesi hiyo.
Yote hayo yalikuwa uongo na ambayo yangewezekana tu kwa sinema.


Alan Knight, alinaswa na polisi kwa camera ya CCTV akisukuma gari la kubebea bidhaa ndani ya duka la Tesco wakati akijidai kuwa mgonjwa mahututi.
Afisaa mmoja wa polisi Paul Harry,kutoka South Wales alisema: ‘Katika kazi yangu hii, sijawahi kuona kisa kama hicho ambacho kilipangwa na kutekelezwa kwa umaakini huo.”
Mkewe Knight mwenye watoto watatu , pia alikuwemo kwenye sakata hiyo kwani siku zote alionekana akimhudumia mumewe aliyejidai kuwa hali mahututi.

141023095919_night_anaswa_na_polisi_512x288_bbc_nocredit
Mbunge wa eneo la Swansea West aliambia BBC kuwa: “Nilikutana na Bi Hellen na akaniarufu ambavyo mumewe alikuwa na hali mbaya ya kiafya na kwamba walitendewa vibaya na polisi.”
Knight anakabiliwa na mashitaka 19 ikiwemo wizi na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela.
Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za ndani na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top