Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kituo cha redio cha Times FM na kampuni ya Times Promotions, wamewasilisha mashtaka mahakamani ya kutaka viongozi wa juu wa Clouds FM pamoja na msanii wa Nigeria, Davido wapelekwe jela kwa kukaidi amri ya mahakama.

Diamond na Davido wakicheza kwa madaha
Kampuni hiyo kupitia wakili wake Peter Kibatala imewasilisha mashtaka hayo katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumatatu hii.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Davido na Clouds FM walikaidi amri ya mahakama iliyotolewa kumtaka Davido asitumbuize kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika October 18 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Times FM walikuwa wameshaingia mkataba na Davido atumbuize November 1 kwenye tamasha lao ambalo linadaiwa kuahirishwa kutokana na kilichotokea.
Soma zaidi habari hiyo iliyoandikwa kwenye gazeti la leo la Daily News hapa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top