STAA wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ amesema kwa mtazamo wake anaona Bongo Movies imebuma
hivyo ameamua kukomaa na shule ili awe na kitu kingine tofauti na sanaa.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Lulu alisema kuwa kwa sasa yuko Chuo
cha Uhazili Magogoni, Posta jijini Dar akichukua ‘course’ ya Utawala wa
Umma (Public Administration) kwa ajili ya kupata ujuzi mwingine
kichwani.
“Mwe-nzangu naona Bongo Movies kunaelekea kubaya, bora hata nikomae
na shule angalau hata niwe na kitu kingine kichwani nipate mbadala wa
sanaa,” alisema Lulu.
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment